January 31, 2010

ADABU ZA KUOMBA DUA

Mwenyezi Mungu S.W.T. na Mtume Wake S.A.W. wametufundisha jinsi ya kutekeleza adabu za kuomba dua wakati Mwislamu anapotaka kuomba dua ili ile dua yake ipate kujibiwa. Kama ifuatavyo:

1.NYAKATI TUKUFU ZINAZOKUBALIWA DUA.
Kuna nyakati maalum ambazo Mwislamu anatakiwa atekeleze ili dua yake ipate kukubaliwa kama vile:
a) Kuomba dua kila baada ya Sala ya Faridha
b) Kuomba dua saa katika siku ya Ijumaa
c) Kuomba dua wakati wa nusu ya usiku au theluthi ya usiku
d) Kuomba dua wakati mtu kafunga na wakati wa kufungua kwa mtu yule aliyefunga
e) Kuomba dua wakati vinapopiganwa vita vya Jihadi kati ya Waislamu na makafiri
f) Kuomba dua wakati inaponyesha mvua
g) Kuomba dua wakati wa kuona L-Ka`aba.
h) Kuomba dua wakati wa kusafiri
i) Kuomba dua wakati Waislamu wamekusanyika katika vikao vya kumdhukuru Mola
j) Kuomba dua wakati wa kunywa maji ya zamzam huko Makka.
k) Kuomba dua wakati wa kutufu (kuizunguka) L-Ka`aba
l) Kuomba dua siku ya Arafah
m) Kuomba dua kwa mtu anayehiji au anayefanya umra.
n) Kuomba dua wakati wa kusimama kwenye Ssafaa na Marwa
o) Kuomba dua katika Laylatul Qadri
p) Kuomba dua kwa mtu aliyedhulumiwa
q) Kuomba dua wakati anapowika jogoo
r) Dua ya mtoto mwema anapomuombea mzazi wake
s) Dua ya mzazi anapomuombea mwanawe
t) Kuomba dua wakati wa kumfumba maiti macho yake
u) Kuomba dua baada ya kutupa mawe kwenye jamra mbili ya kwanza na ya pili.
v) Kuomba dua katika mkusanyiko huko Muzdalifah, baada ya Sala ya Alfajiri
w) Kuomba dua baada ya Adhana
x) Dua ya mtu Mwislamu akimuombea nduguye Mwislamu nyuma ya mgongo wake naye hayupo.

2.KUELEKEA KIBLA NA KUNYOOSHA MIKONO.
Muombaji wakati anapotaka kuomba dua anatakiwa aelekee upande wa kibla na anyooshe mikono yake miwili. Kama alivyosema Mtume S.A.W. katika Hadithi iliyopokelewa na Salmaani L-Farsy R.A.A. na iliyotolewa na Ttirmidhi, “


‘‘إِنَّ اللَّهَ حَيِيٌّ كَرِيمٌ يَسْتَحْيِي إِذَا رَفَعَ الرَّجُلُ إِلَيْهِ يَدَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا’’

Maana yake, “Hakika Mwenyezi Mungu Hai, Mkarimu anaona haya ikiwa mtu atamnyooshea mikono yake airudishe tupu.”
Muombaji akimaliza kuomba dua yake aipanguse mikono yake usoni mwake.Na wala muombaji asipandishe macho yake mbinguni. Kama alivyotukataza Mtume S.A.W. katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na iliyotolewa na Muslim, “

‘‘لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ رَفْعِهِمْ أَبْصَارَهُمْ عِنْدَ الدُّعَاءِ إِلَى السَّمَاءِ أَوْ لَتُخْطَفَنَّ أَبْصَارُهُمْ’’
Maana yake, “Waache watu kupandisha macho yao mbinguni wakati wa kuomba dua au sivyo yatanyakuliwa macho yao.”

3.KUNYENYEKEA NA KUOMBA DUA KWA KHOFU BILA YA KUPAZA SAUTI..
Muombaji anatakiwa asipaze sauti yake wakati wa kuomba dua bali iwe kati na kati. Kwani Mola S.W.T. si kiziwi, anasikia maneno yote yanayosemwa na kila mtu na anaona kila kitu. Na hata anajua nia ya mtu moyoni mwake kabla hata hajaomba dua. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Suratil A`araaf aya ya 205, “
وَاذْكُرْ رَبَّكَ فِي نَفْسِكَ تَضَرُّعًا وَخِيفَةً وَدُونَ الْجَهْرِ مِنْ الْقَوْلِ بِالْغُدُوِّ وَالآصَالِ وَلا تَكُنْ مِنْ الْغَافِلِينَ

Maana yake, “Na mkumbuke Mola wako nafsini kwako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli, asubuhi na jioni. Wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.” Pia kasema katika Suratil Anbiyaa aya ya 90, “

إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ

Maana yake, “…Hakika wao walikuwa wepesi wa kutenda mema, na wakituomba kwa shauku na khofu. Nao walikuwa wakitunyenyekea.”

4.KUWA NA TUMAINI YA KUKUBALIWA DUA.
Muombaji anatakiwa wakati anapoomba dua asiwe na shaka nayo au wasiwasi kwamba labda atakubaliwa au labda atakataliwa. Bali awe na yakini moyoni mwake kwamba Mola atamsaidia na atamkubalia dua yake. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu S.W.T. katika Surat Ghaafir aya ya 60, “

وَقَالَ رَبُّكُمْ ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ...

Maana yake, “Na Mola wenu anasema: “Niombeni nitakujibuni (nitakuitikieni)…”

5..KUTOKATA TAMAA NA KUTOKUFANYA HARAKA KUJIBIWA.
Muuombaji anatakiwa asikate tamaa bali aendelee na kuomba dua na wala asilalamike kwa kusema, “Mbona nimeomba dua lakini sikujibiwa?” Bali awe na subira. Kama alivyotufundisha Mtume wetu S.A.W. kasema katika Hadithi iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. na kutolewa na L-Bukhari, “

‘‘يُسْتَجَابُ لأَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ يَقُولُ: ‘‘دَعَوْتُ فَلَمْ يُسْتَجَبْ لِي’’
Maana yake, “Anakubaliwa mmoja wenu (dua yake) ikiwa hataharakisha kwa kusema, “Nimeomba lakini sikujibiwa.”

6.KUFUNGUA DUA KWA KUMDHUKURU MOLA.
Muombaji anatakiwa aanze kwanza kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha amsalie Mtume S.A.W.., halafu amuombe Mola haja yake na amalizie kwa kumsalia Mtume S.A.W.. Kama vile kusema: “(1)INNA LLAAHA WAMALAAIKATAHU YUSALLUWNA `ALA NABIYYI YA-AYYUHA LLADHIYNA AAMANUW SALLUW `ALAYHI WASALLIMU TASLIYMA: (2)ALLAAHU MASALLI WASALLIM WA BAARIK `ALA SAYYIDINA MUHAMMAD. “(3)RABBANA GHFIRLIY WARHAMNIY INNAKA ANTA TAWWABU RRAHIYMU. (4)WASALLA LLAAHU `ALA SAYYIDINA MUHAMMAD WA`ALA AALIHI WA-AS-HAABIHI AJMA`IYNA


11.DUA YA KUOMBA KUTENGENEKEWA DINI NA DUNIA NA AKHERA.
Mwenye kutaka kutengenekewa na dini yake, na dunia yake, na Akhera yake, na maisha yake na mauti yake, basi aombe dua ifuatayo. Kama ilivyokuja katika Hadithi iliyotolewa na L-Bukhari na iliyopokelewa na Abu Huraira R.A.A. kasema, “Mtume S.A.W. alikuwa akiomba dua ifuatayo, “
‘‘اللَّهُمَّ أَصْلِحْ لِي دِينِي الَّذِي هُوَ عِصْمَةُ أَمْرِي ، وَأَصْلِحْ لِي دُنْيَايَ الَّتِي فِيهَا مَعَاشِي ، وَأَصْلِحْ لِي آخِرَتِي الَّتِي فِيهَا مَعَادِي ، وَاجْعَلِ الْحَيَاةَ زِيَادَةً لِي فِي كُلِّ خَيْرٍ وَاجْعَلِ الْمَوْتَ رَاحَةً لِي مِنْ كُلِّ شَرٍّ’’
“ALLAHUMMA ASLIH LIY DIYNIY LLADHI HUWA `ISMATI AMRIY, WA-ASLIH LIY DUN-YAAYA LLATIY FIYHA MA`AASHIY, WA-ASLIH LIY AAKHIRATIY LLAATIY FIYHA MA`AADIY, WAJ`ALI L-HAYAATA ZIYAADATAN LIY FIY KULLI KHAYRIN WAJ`AL L-MAWTA RAAHATAN LIY MIN KULLI SHARRAN.”
Maana yake, “Ewe Mwenyezi Mungu! Nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo yenye mashikamano yangu, na unitengenezee dunia yangu ambayo ndiyo yenye maisha yangu, na unitengenezee Akhera yangu ambayo ndiyo marejeo yangu, na ujaalie uhai kwangu wa kheri zaidi, na ujaalie mauti kwangu yawe ya raha kutokana na kila shari.”

1 comments:

FARHAD August 12, 2018 at 10:58 AM  

Yalab takabal dua...🙏🙏🙏

  © Blogger templates The Professional Template by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP