August 24, 2011

Laylatul-Qadr (The Night of Power)

Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu?

Tunaingia kumi la mwisho, kumi ambalo ndani yake kuna siku tukufu, siku ya Laylatul-Qadr, ambayo ibada yake ni bora kuliko ibada ya miezi elfu.
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):

﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
(( إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ)) (( وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ)) (( لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ)) ((تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ)) (( سَلَامٌ هِيَ حَتَّى مَطْلَعِ الْفَجْرِ))


BismiLlaahir Rahmaanir Rahiym
((Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatul Qadr, (Usiku wa Makadirio[Majaaliwa]). Na nini kitachokujuulisha nini Laylatul Qadr?)) ((Laylatul-Qadr ni bora kuliko miezi elfu)) ((Huteremka Malaika na Roho (Jibriyl) katika usiku huo kwa idhini ya Mola wao kwa kila jambo)) ((Amani usiku huo mpaka mapambazuko ya alfajiri)) [Al-Qadr: 1-5]

Vile vile dalili katika Hadiyth mbali mbali zimethibiti kuhusu Fadhila za usiku huu mtukufu, na jinsi Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa hali yake katika siku hizi kumi za mwisho za Ramadhaan.

Baada ya kuzijua fadhila zake usiku huu mtukufu inakupasa Muislamu ujikaze katika siku kumi hizi za mwisho kuacha mambo yote yanayokushughulisha ya dunia na utumbukie katika ibada tu ili uweze kuupata usiku huo mtukufu, yaani ukukute wewe ukiwa katika ibada ili zihesabiwe ibada zako kama kwamba umefanya ibada ya miezi elfu.
Tukifanya hesabu miezi elfu hiyo ni sawa na umri wa miaka 83!

1000 ÷ 12 = 83.3 yaani miaka themanini na tatu na miezi mitatu takriban.
Hivyo ikiwa Laylatul-Qadr imekukuta katika ibada ya aina yoyote, ikiwa ni Swalah (Qiyaamul-Layl), kusoma Qur-aan, kufanya aina za dhikr, kutoa sadaka, kulisha chakula, kuwasiliana na jamaa, kujielimisha au kuelimisha, kufanya wema.

KWA FAIDA ZAIDI YA KUHUSU HII LAYLATUL- QUDR TEMBELELEA WWW.ALHIDAAYA.COM

0 comments:

  © Blogger templates The Professional Template by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP